Jumamosi 17 Oktoba 2026 - 08:50
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, Yalaani Hatua za Maafisa wa Azerbaijan na Kusisitiza Haki ya Wasichana Wenye Hijabu Kupata Elimu

Jamhuri ya Azerbaijan ni nchi yenye historia adhimu ya utamaduni wa Kiislamu na kuwapenda Ahlul-Bayt (a.s.). Kwa wanawake na wasichana Waislamu wa nchi hiyo, hijabu ni kielelezo cha imani, utambulisho wa kidini na kushikamana na thamani za Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kutekelezwa sera zinazowekea vikwazo uvaaji wa hijabu na Serikali ya Jamhuri ya Azerbaijan, Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum imetoa taarifa inayowahusu maafisa wa Jamhuri ya Azerbaijan, kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Jamhuri ya Azerbaijan ni nchi yenye historia adhimu ya utamaduni wa Kiislamu na mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s.). Kwa wanawake na wasichana Waislamu wa nchi hiyo, hijabu ni kielelezo cha imani, utambulisho wa kidini na kushikamana na thamani za Kiislamu.

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, ikieleza wasiwasi wake kuhusu vikwazo vilivyowekwa dhidi ya wasichana wanaovaa hijabu, inatarajia kwamba maafisa wa nchi hiyo wataheshimu imani za kidini za wananchi, watakomesha aina yoyote ya kulazimisha watu kuvaa mavazi yasiyozingatia misingi ya dini, na hawataruhusu msichana yeyote kunyimwa haki yake ya kupata elimu na kushiriki katika maisha ya jamii kwa sababu tu ya kushikamana na hijabu ya Kiislamu.

Bila shaka, kuheshimu imani za kidini za wananchi ni ishara ya kuwa na mtazamo wa mbali na ni jambo linaloweka mazingira ya kujenga uaminifu na mshikamano wa kijamii. Imani za kidini haziwezi kung'olewa kutoka katika nyoyo za watu kwa njia ya kulazimisha au kuweka vikwazo. Badala yake, hekima na uvumilivu ni njia inayofaa zaidi ya kuiongoza jamii na kulinda heshima na utu wa binadamu.

Kwa sababu hiyo, kwa nia njema, tunawashauri maafisa wa Jamhuri ya Azerbaijan, ambao wanatangaza kaulimbiu ya uhuru wa kijamii, wapitie upya sera zinazowekea vikwazo uvaaji wa hijabu, waheshimu haki za kidini za Waislamu, na waweke mazingira yatakayowawezesha wasichana wanaovaa hijabu kupata elimu na kuishi kwa heshima, utulivu na amani.

Tunatumaini kwamba, kupitia busara na kuheshimiana, njia ya kulinda thamani za Kiislamu, kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kuhifadhi haki za wananchi itafunguliwa na kuwa rahisi zaidi.

Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha